Leviticus 2:1
“ ‘Mtu yeyote aletapo sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 2:4“ ‘Kama utaleta sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni, itakuwa ya unga laini: maandazi yaliyotengenezwa bila kutiwa chachu, yaliyochanganywa na mafuta, au mikate myembamba iliyotengenezwa bila kutiwa chachu, na iliyopakwa mafuta.
Leviticus 5:11“ ‘Ikiwa basi, hawezi kupata hua wawili au makinda mawili ya njiwa, ataleta sehemu ya kumi ya efa + 5:11 Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja. ya unga laini kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kamwe asiweke mafuta wala uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya dhambi.
Leviticus 6:14“ ‘Haya ndiyo masharti ya sadaka ya nafaka: Wana wa Aroni wataileta mbele za Bwana, mbele za madhabahu.
Leviticus 7:10Nayo kila sadaka ya nafaka, iwe imechanganywa na mafuta au iko kavu, itakuwa ya wana wa Aroni, nayo itagawanywa sawa kati yao. 1 Sadaka Ya Amani
Leviticus 9:17Pia akaleta sadaka ya nafaka, akachukua konzi moja na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi.
Leviticus 24:7Kando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto.