Leviticus 23:5
Pasaka ya Bwana huanza jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In the fourteenth day of the first month at even is the LORD’S passover.
In Context
Cross References
Exodus 12:11Hivi ndivyo mtakavyokula: Mtajifunga mikanda viunoni, mtakuwa mmevaa viatu vyenu miguuni na kushika fimbo zenu mkononi mwenu. Mle kwa haraka; hii ni Pasaka ya Bwana.
Exodus 13:3Ndipo Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu Bwana aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu.
Numbers 9:2“Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamriwa.
Deuteronomy 16:1Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka ya Bwana Mungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku.
2 Chronicles 35:18Kulikuwa hakujafanyika Pasaka kama hii katika Israeli tangu siku za nabii Samweli wala hakukuwa na mfalme yeyote wa Israeli ambaye kamwe alishaadhimisha Pasaka kama ile aliyofanya Mfalme Yosia, akiwa na makuhani, Walawi na watu wote wa Yuda na watu wa Israeli waliokuwepo huko, pamoja na watu wa Yerusalemu.
Mark 14:12Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo kwa desturi mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wa Yesu wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”