Luke 1:32
Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanaume na utamwita jina lake Yesu.
33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”
Cross References
2 Samuel 7:16Nyumba yako na ufalme wako utadumu milele mbele zangu, kiti chako cha enzi kitafanywa imara milele.’ ”
Isaiah 9:6Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, 2 tumepewa mtoto mwanaume, 2 nao utawala utakuwa mabegani mwake. 1 Naye ataitwa 2 Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, 2 Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. 1
Jeremiah 23:5Bwana asema, “Siku zinakuja, 2 nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki, 1 Mfalme atakayetawala kwa hekima, 2 na kutenda lililo haki na sawa katika nchi. 1
Ezekiel 17:22“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kwenye kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana.
Ezekiel 37:24“ ‘Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja. Watafuata sheria zangu na kuzishika amri zangu kwa uangalifu.
Matthew 1:1Habari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu: 1