Luka 11:31
Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kuwahukumu watu wa kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Solomoni. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Solomoni.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Kings 10:1Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Solomoni na uhusiano wake na jina la Bwana, akaja kumjaribu kwa maswali magumu.
Isaiah 9:6Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, 2 tumepewa mtoto mwanaume, 2 nao utawala utakuwa mabegani mwake. 1 Naye ataitwa 2 Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, 2 Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. 1
Jeremiah 3:11Bwana akaniambia, “Israeli asiye mwaminifu ana haki kuliko Yuda mdanganyifu.
Luke 3:22Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.” 1 Ukoo Wa Bwana Yesu (Mathayo 1:1-17)
Romans 2:27Ndipo wale ambao hawakutahiriwa kimwili lakini wanaitii sheria watawahukumu ninyi, ambao ingawa mmetahiriwa na kuijua sana sheria ya Mungu iliyoandikwa, lakini mwaivunja.
Hebrews 11:7Kwa imani, Noa alipoonywa na Mungu kuhusu mambo ambayo hayajaonekana bado, kwa kumcha Mungu alitengeneza safina ili kuokoa jamaa yake. Kwa imani yake aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani. 1 Imani Ya Abrahamu