Luka 12:15
Ndipo Yesu akawaambia, “Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
14Lakini Yesu akamwambia, “Rafiki, ni nani aliyeniweka mimi kuwa hakimu wenu au msuluhishi juu yenu?”
16Kisha akawaambia mfano huu: “Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana.
Cross References
Joshua 7:21Nilipoona katika nyara joho zuri la kutoka Babeli, shekeli mia mbili + 7:21 Shekeli 200 za fedha ni sawa na kilo 2.3. za fedha, na kabari ya dhahabu ya uzito wa shekeli hamsini, + 7:21 Shekeli 50 ni sawa na gramu 600. nikavitamani na nikavichukua. Tazama, vimefichwa ardhini ndani ya hema langu, pamoja na hiyo fedha chini yake.”
Job 2:4Shetani akamjibu Bwana, “Ngozi kwa ngozi! Mwanadamu atatoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya uhai wake.
Psalms 10:3Hujivunia tamaa za moyo wake; 2 humbariki mlafi na kumtukana Bwana. 1
Psalms 62:10Usitumainie vya udhalimu 2 wala usijivune kwa vitu vya wizi; 1 ingawa utajiri wako utaongezeka, 2 usiviwekee moyo wako. 1
Proverbs 15:16Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana, 2 kuliko mali nyingi pamoja na ghasia. 1
Proverbs 23:4Usijitaabishe ili kuupata utajiri, 2 uwe na hekima kuonyesha kujizuia. 1