Luke 21:25
“Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Hapa duniani, mataifa yatakuwa katika dhiki na fadhaa kutokana na ngurumo na misukosuko ya bahari.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 46:3Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka, 2 milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake. 1
Isaiah 5:30Katika siku ile watanguruma juu yake 2 kama ngurumo za bahari. 1 Kama mtu akiitazama nchi, 2 ataona giza na dhiki; 2 hata nuru itatiwa giza kwa mawingu.
Isaiah 13:13Kwa hiyo nitazifanya mbingu zitetemeke, 2 nayo dunia itatikisika kutoka mahali pake 1 katika ghadhabu ya Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 katika siku ya hasira yake iwakayo. 1
Isaiah 24:23Mwezi utatiwa haya, nalo jua litaaibishwa; 2 kwa maana Bwana Mwenye Nguvu Zote atawala 1 juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu, 2 tena mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Jeremiah 4:23Niliitazama dunia, 2 nayo haikuwa na umbo tena ni tupu; 1 niliziangalia mbingu, 2 mianga ilikuwa imetoweka. 1
Daniel 12:1“Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa.