Luke 21:6
“Kuhusu haya mnayoyaona hapa, wakati utafika ambapo hakuna jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.” 1 Mateso (Mathayo 24:3-14; Marko 13:3-13)
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Chronicles 7:20ndipo nitakapoingʼoa Israeli kutoka nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote.
Jeremiah 7:11Je, nyumba hii, iitwayo kwa Jina langu, imekuwa pango la wanyangʼanyi kwenu? Lakini nimekuwa nikiona yanayotendeka! asema Bwana.
Jeremiah 26:9Kwa nini unatoa unabii katika jina la Bwana kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa na kuachwa tupu?” Nao watu wote wakamkusanyikia na kumzunguka Yeremia ndani ya nyumba ya Bwana.
Lamentations 2:6Ameharibu maskani yake kama bustani, 2 ameharibu mahali pake pa mkutano. 1 Bwana amemfanya Sayuni kusahau 2 sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; 1 katika hasira yake kali amewadharau 2 mfalme na kuhani. 1
Lamentations 5:18kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa, 2 nao mbweha wanatembea juu yake. 1
Daniel 9:26Baada ya majuma sitini na mawili, Mpakwa Mafuta atakatiliwa mbali, wala hatabaki na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea mpaka mwisho, nao ukiwa umeamriwa.