Luka 5:14
Yesu akamwagiza akisema, “Usimwambie mtu yeyote, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani na ukatoe sadaka alizoagiza Mose kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 13:2“Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe au upele au alama nyeupe juu ya ngozi yake ambayo yaweza kuwa ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, + 13:2 Ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, yaani ukoma, ni neno lililotumika kwa Kiebrania kueleza magonjwa mbalimbali ya ngozi ambayo si lazima yawe ni ukoma halisi. ni lazima aletwe kwa Aroni kuhani ama kwa wanawe, kuhani mmojawapo.
Matthew 8:4Kisha Yesu akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Mose, ili kuwa ushuhuda kwao.” 1 Yesu Amponya Mtumishi Wa Jemadari (Luka 7:1-10)
Matthew 10:18Nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na kwa watu wa Mataifa.
Mark 1:44akimwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote habari hizi, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka alizoagiza Mose kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.”
Luke 9:5Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”