Luke 7:38
Yule mwanamke akasimama nyuma ya miguu ya Yesu akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake, akaibusu na kuimiminia manukato.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Judges 2:4Malaika wa Bwana alipomaliza kusema mambo haya kwa Waisraeli wote, watu wakalia kwa sauti kuu.
Psalms 6:6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; 2 usiku kucha nafurikisha 2 kitanda changu kwa machozi; 1 nimelowesha viti vyangu vya fahari 2 kwa machozi. 1
Psalms 51:17Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, 2 moyo uliovunjika wenye toba, 2 Ee Mungu, hutaudharau. 1
Ecclesiastes 9:8Daima uvae nguo nyeupe na daima upake kichwa chako mafuta.
Isaiah 57:9Ulikwenda kwa Moleki + 57:9 Moleki alikuwa mungu aliyekuwa anaabudiwa na Waamoni; pia alijulikana kama Malkomu, Maloki au Kemoshi wa Moabu. ukiwa na mafuta ya zeituni, 2 na ukaongeza manukato yako. 1 Ukawatuma wajumbe wako mbali sana, 2 ukashuka kwenye kaburi + 57:9 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. lenyewe! 1
Jeremiah 31:9Watakuja wakilia; 2 wataomba wakati ninawarudisha. 1 Nitawaongoza kando ya vijito vya maji 2 katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa, 1 kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli, 2 naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza. 1