Luke 8:32
Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo likilisha kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Kings 22:22“ Bwana akauliza, ‘Kwa njia gani?’ “Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’ “ Bwana akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’
Job 1:12Bwana akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.” Ndipo Shetani akatoka mbele za Bwana.
Psalms 62:11Jambo moja Mungu amelisema, 2 mambo mawili nimeyasikia: 1 kwamba, Ee Mungu, 2 wewe una nguvu, 1
Isaiah 66:3Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali 2 ni kama yeye auaye mtu, 1 na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, 2 ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. 1 Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, 2 ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, 1 na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, 2 ni kama yule aabuduye sanamu. 1 Wamejichagulia njia zao wenyewe, 2 nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao. 1
Mark 5:11Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe lililokuwa likilisha karibu kando ya kilima.
1 John 4:4Watoto wapendwa, ninyi mmetokana na Mungu, nanyi mmewashinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu.