Malachi 1:7
“Mnatoa sadaka chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu. “Lakini ninyi mnauliza, ‘Tumekutia unajisi kwa namna gani?’ “Kwa kusema kuwa meza ya Bwana ni ya kudharauliwa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 2:11“ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa Bwana ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka itolewayo kwa Bwana kwa moto.
Deuteronomy 15:21Kama mnyama ana dosari, akiwa ni kilema au kipofu au kama ana kilema kibaya, kamwe usimtoe dhabihu kwa Bwana Mungu wenu.
Ezekiel 41:22Kulikuwa na madhabahu ya mbao kimo chake dhiraa tatu na ilikuwa dhiraa mbili mraba pande zote, tako lake na pande zake zilikuwa za mbao. Yule mtu akaniambia, “Hii ni meza ambayo iko mbele za Bwana.”
Malachi 1:12“Lakini mnalinajisi Jina langu kwa kusema kuhusu meza ya Bwana, ‘Imetiwa unajisi pamoja na chakula chake. Ni ya kudharauliwa.’
1 Corinthians 11:21kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anakula bila kuwangoja wengine. Mmoja hukaa njaa na mwingine analewa.