Mark 1:45
Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo, Yesu hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi lakini alikaa sehemu zisizo na watu. Hata hivyo watu wakamfuata huko kutoka kila upande.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 77:11Nitayakumbuka matendo ya Bwana; 2 naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. 1
Matthew 28:15Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha nao wakafanya kama walivyoelekezwa. Habari hii imeenea miongoni mwa Wayahudi mpaka leo. 1 Yesu Awatuma Wanafunzi Wake (Marko 16:14-18; Luka 24:36-49; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)
Mark 2:13Yesu akaenda tena kandokando ya Bahari ya Galilaya. Umati mkubwa wa watu ukamfuata, naye akaanza kuwafundisha.
Luke 5:15Lakini habari zake Yesu zikazidi sana kuenea kotekote kuliko wakati mwingine wowote. Makutano makubwa ya watu yalikuwa yakikusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Titus 1:10Kwa maana wako wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, hasa wale wa kikundi cha tohara.