Mark 5:15
Walipofika kwa Yesu, wakamwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu legioni akiwa ameketi hapo, amevaa nguo na mwenye akili timamu. Wakaogopa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 16:4Samweli akafanya kile Bwana alichosema. Alipofika Bethlehemu, wazee wa mji wakatetemeka walipomlaki. Wakauliza, “Je, umekuja kwa amani?”
1 Chronicles 15:13Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la Bwana mara ya kwanza, hata ikasababisha Bwana Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.”
Psalms 14:5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu, 2 maana Mungu yupo pamoja na wenye haki. 1
Matthew 4:24Kwa hiyo sifa zake zikaenea sehemu zote za Shamu, nao watu wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na maumivu, waliopagawa na pepo wachafu, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya.
Matthew 12:29“Au tena, mtu awezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akishamfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali zake.
Mark 5:9Yesu akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Jina langu ni Legioni, + 5:9 Legioni maana yake ni Jeshi. kwa kuwa tuko wengi.”