Mark 6:21
Mfalme Herode alifanya karamu kubwa wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake. Akawaalika maafisa wake wakuu, majemadari wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. Hatimaye Herodia alipata wasaa aliokuwa akiutafuta.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 40:20Mnamo siku ya tatu, ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake:
Esther 1:3Katika mwaka wa tatu wa utawala wake, alifanya karamu kwa ajili ya wakuu wake wote pamoja na maafisa. Akawaalika viongozi wa jeshi wa Uajemi na Umedi, wana wa wafalme na wakuu wa majimbo.
Esther 3:7Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa Mfalme Ahasuero, katika mwezi wa kwanza uitwao Nisani, walipiga puri (yaani kura) mbele ya Hamani ili kuchagua siku na mwezi. Kura ikaangukia kwenye mwezi wa kumi na mbili, yaani Adari.
Proverbs 31:4“Ee Lemueli, haifai wafalme, 2 haifai wafalme kunywa mvinyo, 2 haifai watawala kutamani sana kileo, 1
Hosea 7:5Katika sikukuu ya mfalme wetu 2 wakuu wanawaka kwa mvinyo, 2 naye anawaunga mkono wenye mizaha. 1
Acts 12:2Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga.