Mark 7:9
Naye akawaambia, “Ninyi mnayo njia nzuri ya kukataa amri za Mungu ili mpate kuyashika mapokeo yenu!
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
8Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushika desturi za watu.”
Cross References
Psalms 119:126Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia, 2 kwa kuwa sheria yako inavunjwa. 1
Isaiah 29:13Bwana anasema: 1 “Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao 2 na kuniheshimu kwa midomo yao, 2 lakini mioyo yao iko mbali nami. 1 Ibada yao kwangu inatokana na maagizo 2 waliyofundishwa na wanadamu. 1
Daniel 7:25Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake, huku akijaribu kubadili majira na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati. + 7:25 Wakati, nyakati mbili, na nusu wakati maana yake ni mwaka mmoja, miaka miwili, na nusu mwaka, yaani miaka mitatu na nusu.
Matthew 15:3Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
Mark 7:13Kwa njia hiyo ninyi mnabatilisha neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyojiwekea. Nanyi mnafanya mambo mengi ya aina hiyo.”
Galatians 2:21Siibatilishi neema ya Mungu, kwa maana kama haki ingeweza kupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure!”