Mark 8:38
Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
37Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Cross References
Daniel 7:10Mto wa moto ulikuwa unatiririka, 2 ukipita mbele yake. 1 Maelfu elfu wakamhudumia; 2 kumi elfu mara kumi elfu wakasimama mbele zake. 1 Mahakama ikakaa kuhukumu, 2 na vitabu vikafunguliwa.
Zechariah 14:5Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha Bwana Mungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye.
Matthew 10:32“Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi nami nitamkiri yeye mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
Matthew 13:41Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote.
Matthew 16:27Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Matthew 25:31“Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu wake.