Matthew 13:32
Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hadi ndege wa angani wanakuja na kutengeneza viota katika matawi yake.” 1 Mfano Wa Chachu (Luka 13:20-21)
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 72:16Nafaka ijae tele katika nchi yote, 2 juu ya vilele vya vilima na istawi. 1 Tunda lake na listawi kama Lebanoni, 2 listawi kama majani ya kondeni. 1
Isaiah 2:2Katika siku za mwisho 1 mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa 2 kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, 1 utainuliwa juu ya vilima, 2 na mataifa yote yatamiminika huko.
Ezekiel 31:6Ndege wote wa angani 2 wakaweka viota kwenye vitawi vyake, 1 wanyama wote wa shambani 2 wakazaana chini ya matawi yake, 1 mataifa makubwa yote 2 yaliishi chini ya kivuli chake. 1
Daniel 2:34Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo wa mfinyanzi, na kuivunja.
Daniel 4:12Majani yake yalikuwa ya kupendeza, matunda yake yalikuwa mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Chini ya kivuli chake wanyama wa kondeni walipata hifadhi, na ndege wa angani waliishi katika matawi yake. Kila kiumbe kililishwa kutokana na mti huo.
Zechariah 4:10“Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli. “(Hizi saba ni macho ya Bwana ambayo huzunguka duniani kote.)”