Mathayo 15:31
Hao watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona, wakamtukuza Mungu wa Israeli. 1 Yesu Alisha Watu Elfu Nne (Marko 8:1-10)
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 33:20Pale akajenga madhabahu na kupaita El-Elohe-Israeli. + 33:20 El-Elohe-Israeli maana yake Mungu, Mungu wa Israeli au Mwenye Nguvu ni Mungu wa Israeli.
Psalms 50:15na uniite siku ya taabu; 2 nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”
Matthew 9:8Makutano walipoyaona haya, wakajawa na hofu ya Mungu, wakamtukuza Mungu ambaye alikuwa ametoa mamlaka kama haya kwa wanadamu. 1 Kuitwa Kwa Mathayo (Marko 2:13-17; Luka 5:27-32)
Matthew 18:8Ikiwa mkono wako au mguu wako unakusababisha utende dhambi, ukate na uutupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa huna mkono mmoja au mguu mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.
Mark 2:12Yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama, akachukua mkeka wake, akatembea machoni pao wote! Jambo hili likawashangaza wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, “Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!” 1 Yesu Amwita Lawi (Mathayo 9:9-13; Luka 5:27-32)
Mark 9:43Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki. [