Matthew 2:7
Ndipo Herode akawaita wale wataalamu wa nyota kwa siri na kutaka kujua kutoka kwao uhakika kamili wa wakati ile nyota ilionekana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 18:21Sauli akawaza, “Nitampa Daudi binti yangu, ili apate kuwa mtego kwake, ili kwamba mkono wa Wafilisti upate kuwa juu yake.” Hivyo Sauli akamwambia Daudi, “Sasa unayo nafasi ya pili ya kuwa mkwe wangu.”
Psalms 55:21Mazungumzo yake ni laini kama siagi, 2 hata hivyo vita vimo moyoni mwake. 1 Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, 2 hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa. 1
Psalms 83:3Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako, 2 wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda. 1
Ezekiel 38:10“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya.
Revelation 12:1Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ukiwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake.