Matthew 20:1
“Kwa maana Ufalme wa Mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba aliyetoka alfajiri ili kwenda kuajiri vibarua kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Song of Solomon 8:11Solomoni alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni; 2 alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji. 1 Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake 2 shekeli 1,000 + 8:11 Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5. za fedha. 1
Jeremiah 25:3Kwa miaka ishirini na mitatu, kuanzia mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, hadi siku hii ya leo, neno la Bwana limekuwa likinijia, nami nimesema nanyi mara kwa mara, lakini hamkusikiliza.
Matthew 9:37Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache.
Matthew 13:31Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa Mbinguni ni kama punje ya haradali, ambayo mtu aliichukua, akaipanda shambani mwake.
Matthew 13:44“Ufalme wa Mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.”
Matthew 21:28“Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Akamwendea yule wa kwanza akamwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’