Matthew 21:33
“Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo ndani yake na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka, akasafiri kwenda nchi nyingine.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 1:15Kwa hiyo niliwachukua wanaume viongozi wa makabila yenu, wenye hekima na wanaoheshimika, nami nikawateua wawe na mamlaka juu yenu kama majemadari wa maelfu, wa mamia, wa hamsini, na wa makumi, na kama maafisa wa makabila.
Deuteronomy 17:9Nendeni kwa makuhani, ambao ni Walawi, na kwa mwamuzi ambaye atakuwa kazini wakati huo. Ulizeni kwao nao watawapa maamuzi.
1 Kings 22:19Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Bwana: Nilimwona Bwana ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka upande wa kulia na wa kushoto.
Song of Solomon 8:11Solomoni alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni; 2 alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji. 1 Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake 2 shekeli 1,000 + 8:11 Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5. za fedha. 1
Isaiah 5:1Nitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye, 2 kuhusu shamba lake la mizabibu: 1 Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu 2 kwenye kilima chenye rutuba. 1
Jeremiah 19:3nawe useme, ‘Sikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda na watu wa Yerusalemu. Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Sikilizeni! Nitaleta maafa mahali hapa, ambayo yatafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yawashe.