Matthew 5:29
Jicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa jehanamu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Proverbs 5:8Njia zenu ziwe mbali naye, 2 msiende karibu na mlango wa nyumba yake, 1
Matthew 10:28Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu. + 10:28 Jehanamu kwa Kiyunani ni Gehena, maana yake ni Kuzimu, yaani motoni.
Matthew 18:8Ikiwa mkono wako au mguu wako unakusababisha utende dhambi, ukate na uutupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa huna mkono mmoja au mguu mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.
Matthew 23:15“Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, enyi wanafiki! Ninyi mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja mwongofu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya mwana wa jehanamu mara mbili kuliko ninyi!
Mark 8:36Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake?
Luke 9:24Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.