Numbers 16:5
Kisha akamwambia Kora na wafuasi wake wote: “Asubuhi Bwana ataonyesha ni nani aliye wake na ni nani aliye mtakatifu, tena atamtaka mtu huyo aje kwake. Mtu yule ambaye atamchagua atamfanya kuja karibu naye.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
4Mose aliposikia jambo hili, akaanguka kifudifudi.
6Wewe Kora na wafuasi wako wote mtafanya hivi: Chukueni vyetezo,
Cross References
Exodus 28:1“Mtwae Aroni ndugu yako aliyeletwa kwako kutoka miongoni mwa Waisraeli, pamoja na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
Exodus 28:43Aroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake.
Leviticus 10:3Kisha Mose akamwambia Aroni, “Hili ndilo alilonena Bwana wakati aliposema: 1 “ ‘Miongoni mwa wale watakaonikaribia 2 nitajionyesha kuwa mtakatifu; 1 machoni pa watu wote 2 nitaheshimiwa.’ ” Aroni akanyamaza.
Leviticus 21:12wala asiondoke mahali patakatifu pa Mungu wake au kupanajisi, kwa sababu amewekwa wakfu kwa mafuta ya Mungu wake. Mimi ndimi Bwana.
Numbers 17:5Fimbo ya mtu nitakayemchagua itachipuka, nami mwenyewe nitayakomesha haya manungʼuniko ya mara kwa mara ya Waisraeli dhidi yako.”
Psalms 65:4Heri wale uliowachagua 2 na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako! 1 Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako, 2 mema ya Hekalu lako takatifu. 1