Numbers 34:3
“ ‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, + 34:3 Yaani Bahari Mfu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 23:31“Nitaweka mipaka ya nchi yako kuanzia Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kuanzia jangwani hadi Mto Frati. Nitawatia watu wanaoishi katika nchi hizo mikononi mwako, nawe utawafukuza watoke mbele yako.
Joshua 3:16maji hayo yaliyotiririka kutoka upande wa juu yaliacha kutiririka yakasimama kama chuguu mbali kabisa nao, kwenye mji ulioitwa Adamu kwenye eneo la Sarethani, wakati yale maji yaliyokuwa yanatiririka kuingia kwenye Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), yalitindika kabisa. Hivyo watu wakavuka kukabili Yeriko.
Ezekiel 47:8Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka mpaka Araba, + 47:8 Araba hapa ina maana ya Bonde la Yordani. ambapo huingia Baharini. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari, + 47:8 Bahari hapa ina maana ya Bahari ya Chumvi. maji yaliyoko humo huponywa na kuwa safi.
Ezekiel 47:18Upande wa mashariki mpaka utapita kati ya Haurani na Dameski, kuambaa Yordani na kati ya Gileadi na nchi ya Israeli, hadi bahari ya mashariki + 47:18 Bahari ya mashariki hapa ina maana ya Bahari ya Chumvi. na kufika Tamari. Huu utakuwa ndio mpaka wa mashariki. 1