Proverbs 18:24
Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu, 2 bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
23Mtu maskini huomba kuhurumiwa 2 bali tajiri hujibu kwa ukali. 1
Cross References
1 Samuel 18:3Yonathani akafanya agano na Daudi kwa sababu alimpenda kama nafsi yake mwenyewe.
1 Samuel 30:26Daudi alipofika Siklagi, akatuma baadhi ya nyara kwa wazee wa Yuda, waliokuwa rafiki zake, akasema, “Tazama, hapa kuna zawadi kwa ajili yenu kutoka nyara za adui za Bwana.”
2 Samuel 9:1Daudi akauliza, “Je, hakuna mtu hata mmoja wa nyumba ya Sauli aliyebaki ambaye naweza kumtendea wema kwa ajili ya Yonathani?”
2 Samuel 16:17Absalomu akamuuliza Hushai, “Je, huu ndio upendo unaomwonyesha rafiki yako? Kwa nini hukufuatana na rafiki yako?”
2 Samuel 19:30Mefiboshethi akamwambia mfalme, “Mruhusu achukue kila kitu, kwa kuwa sasa bwana wangu mfalme amerudi nyumbani salama.”
1 Chronicles 12:38Wote hawa walikuwa watu wapiganaji waliojitolea kutumika katika safu zao. Walikuja Hebroni wakiwa wameamua kikamilifu kumfanya Daudi mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wengine wote walikuwa pia na nia hiyo moja ya kumfanya Daudi kuwa mfalme.