Ufunuo 2:24
“Lakini ninyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezabeli, na ambao hamkujifunza kile wanachokiita Siri ya Shetani, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.
Biblia Takatifu
In The King James Version
In Context
25Lazima mzingatie yale mliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja.
Cross References
Acts 15:28Basi, Roho Mtakatifu na sisi tumekubali tusiwatwike mzigo zaidi ya mambo haya muhimu:
2 Corinthians 2:11ili tusimpe nafasi Shetani atudanganye; maana twaijua mipango yake ilivyo.
2 Corinthians 11:13Maana, hao ni mitume wa uongo, wafanyakazi wadanganyifu wanojisingizia kuwa mitume wa Kristo.
2 Thessalonians 2:9Huyo Mwovu atakuja na nguvu za Shetani na kufanya kila namna ya miujiza na maajabu ya uongo,
Revelation 13:14Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena.