Ufunuo 20:13
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, nayo mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Kila mtu akahukumiwa kulingana na yale aliyoyatenda.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 26:19Lakini wafu wenu wataishi, 2 nayo miili yao itafufuka. 1 Ninyi mnaokaa katika mavumbi, 2 amkeni mkapige kelele kwa furaha. 1 Umande wenu ni kama umande wa asubuhi, 2 dunia itawazaa wafu wake. 1
John 5:28“Msishangae kusikia haya, kwa maana saa inakuja ambapo wale walio makaburini wataisikia sauti yake.
Revelation 1:18Mimi ni Yeye Aliye Hai, niliyekuwa nimekufa, na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu. + 1:18 Kuzimu linalotokana na neno Hades la Kiyunani au Sheol kwa Kiebrania; maana yake ni mahali pa mateso kwa watu waliopotea.
Revelation 20:12Nami nikawaona wafu wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni kitabu cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao kama yalivyoandikwa ndani ya hivyo vitabu.