Ufunuo 22:2
kupitia katikati ya barabara kuu ya huo mji. Kwenye kila upande wa huo mto kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, ukizaa matunda yake kila mwezi. Nayo majani ya mti huo ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 2:9Bwana Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya.
Psalms 147:3Anawaponya waliovunjika mioyo 2 na kuvifunga vidonda vyao. 1
Isaiah 6:10Fanya mioyo ya watu hawa kuwa migumu, 2 fanya masikio yao yasisikie, 2 na upofushe macho yao. 1 Wasije wakaona kwa macho yao, 2 na wakasikiliza kwa masikio yao, 2 wakaelewa kwa mioyo yao, 1 nao wakageuka, nikawaponywa.”
Jeremiah 17:14Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka; 2 uniokoe nami nitaokoka, 2 kwa maana wewe ndiwe ninayekusifu. 1
Ezekiel 47:8Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka mpaka Araba, + 47:8 Araba hapa ina maana ya Bonde la Yordani. ambapo huingia Baharini. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari, + 47:8 Bahari hapa ina maana ya Bahari ya Chumvi. maji yaliyoko humo huponywa na kuwa safi.
Malachi 4:2Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.