Romans 13:4
Kwa maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema. Lakini kama ukitenda mabaya, basi ogopa, kwa kuwa hauinui upanga bila sababu. Yeye ni mtumishi wa Mungu, mjumbe wa Mungu wa kutekeleza adhabu juu ya watenda mabaya.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Joshua 20:5Kama mlipiza kisasi wa damu akimfuatilia, wasimkabidhi yule mshtakiwa, kwa sababu alimuua jirani yake bila kukusudia, na bila kuwa na nia ya kudhuru.
1 Kings 10:9Ahimidiwe Bwana Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe na kukuweka juu ya kiti cha ufalme cha Israeli. Kwa sababu ya upendo wake Bwana wa milele ajili ya Israeli, amekufanya mfalme, ili kudumisha haki na uadilifu.”
Psalms 82:2“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki 2 na kuonyesha upendeleo kwa waovu? 1
Proverbs 20:2Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; 2 yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake. 1
Proverbs 20:26Mfalme mwenye hekima hupepeta waovu, 2 hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao. 1
Proverbs 31:8“Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea, 2 kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa. 1