Romans 4:13
Kwa maana ile ahadi kwamba angeurithi ulimwengu haikuja kwa Abrahamu au kwa wazao wake kwa njia ya sheria bali kwa njia ya haki ipatikanayo kwa imani.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
14Kwa maana ikiwa wale waishio kwa sheria ndio warithi, imani haina thamani na ahadi haifai kitu,
Cross References
Genesis 17:4“Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi.
Genesis 22:17hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,
Genesis 49:10Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, 2 wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, 1 hadi aje yeye ambaye milki ni yake, 2 ambaye utii wa mataifa ni wake. 1
Psalms 72:11Wafalme wote watamsujudia 2 na mataifa yote yatamtumikia. 1
Galatians 3:16Ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Maandiko hayasemi “kwa wazao,” likimaanisha watu wengi, bali “kwa mzao wako,” yaani mtu mmoja, ndiye Kristo.