Romans 5:19
Kwa maana kama vile kwa kutokutii kwa yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 53:10Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana 2 kumchubua na kumsababisha ateseke. 1 Ingawa Bwana amefanya maisha yake 2 kuwa sadaka ya hatia, 1 ataona uzao wake na kuishi siku nyingi, 2 nayo mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake. 1
Romans 5:12Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja, na kupitia dhambi hii mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi:
Romans 5:18Kwa hiyo, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta adhabu kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la haki la mtu mmoja lilileta kuhesabiwa haki ambako huleta uzima kwa wote.
Ephesians 1:6Kwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia sisi katika Mwanawe Mpendwa.
Revelation 7:9Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao.