Romans 8:24
Kwa kuwa tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alicho nacho tayari?
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
25Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatuna, basi twakingojea kwa saburi.
Cross References
Psalms 33:18Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao, 2 kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo, 1
Psalms 146:5Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, 2 ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake, 1
Jeremiah 17:7“Lakini amebarikiwa mtu ambaye tumaini lake ni katika Bwana, 2 ambaye matumaini yake ni katika Bwana. 1
Romans 5:2ambaye kwa kupitia kwake tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo ndani yake sasa tunasimama, nasi twafurahia katika tumaini letu la kushiriki utukufu wa Mungu.
Romans 15:4Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.
1 Corinthians 13:13Basi sasa, yanadumu mambo haya matatu: Imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu miongoni mwa haya matatu ni upendo.