Zekaria 10:11
Watapita katika bahari ya mateso; 2 bahari iliyochafuka itatulizwa 2 na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka. 1 Kiburi cha Ashuru kitashushwa, 2 nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
12Nitawaimarisha katika Bwana, 2 na katika jina lake watatembea,” 4 asema Bwana.
Cross References
Genesis 8:1Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka.
Exodus 14:27Mose akanyoosha mkono wake juu ya bahari, wakati wa mapambazuko bahari ikarudiana na kuwa kama kawaida. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji, lakini Bwana akawasukumia ndani ya bahari.
2 Kings 2:8Eliya akachukua vazi lake, akalisokota na kupiga nalo maji. Maji yakagawanyika upande wa kuume na upande wa kushoto, nao wawili wakavuka pakavu.
Ezra 6:22Kwa muda wa siku saba waliiadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa furaha, kwa sababu Bwana alikuwa amewajaza furaha kwa kubadilisha nia ya mfalme wa Ashuru kwamba awasaidie ujenzi wa nyumba ya Mungu, Mungu wa Israeli.
Psalms 77:16Maji yalikuona, Ee Mungu, 2 maji yalikuona yakakimbia, 2 vilindi vilitetemeka. 1
Psalms 114:5Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, 2 nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma, 1