Zekaria 6:5
Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
4Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?”
Cross References
1 Kings 19:11Bwana akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za Bwana, kwa kuwa Bwana yu karibu kupita hapo.” Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za Bwana, lakini Bwana hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakini Bwana hakuwamo kwenye lile tetemeko.
2 Chronicles 18:18Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Bwana: Nilimwona Bwana ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama upande wa kulia na wa kushoto.
Job 2:1Siku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele za Bwana. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake.
Psalms 104:3na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. 1 Huyafanya mawingu kuwa gari lake, 2 na hupanda kwenye mbawa za upepo. 1
Psalms 148:8umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, 2 pepo za dhoruba zinazofanya amri zake, 1
Ezekiel 1:5Katika ule moto kulikuwa na kitu kinachofanana na viumbe vinne vyenye uhai. Katika kuonekana kwake vilikuwa na umbo mfano wa mwanadamu,