Sefania 2:7
Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda, 2 hapo watapata malisho. 1 Wakati wa jioni watajilaza chini 2 katika nyumba za Ashkeloni. 1 Bwana Mungu wao atawatunza, 2 naye atawarudishia wafungwa wao. 1 Dhidi Ya Moabu Na Amoni 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 50:24Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ninakaribia kufa. Lakini kwa hakika Mungu atawasaidia na kuwachukueni kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyomwahidi kwa kiapo Abrahamu, Isaki na Yakobo.”
Psalms 85:1Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. 2 Ulimrejeshea Yakobo baraka zake. + 85:1 Au: Uliwarudisha mateka wa Yakobo. 1
Isaiah 11:11Katika siku hiyo Bwana atanyoosha mkono wake mara ya pili kurudisha mabaki ya watu wake waliosalia kutoka Ashuru, Misri, Pathrosi, + 11:11 Pathrosi ina maana Misri ya Juu. Kushi, Elamu, Babeli, Hamathi na kutoka visiwa vya baharini. 1
Isaiah 14:1Bwana atamhurumia Yakobo, 2 atamchagua Israeli tena, 2 na kuwakalisha katika nchi yao wenyewe. 1 Wageni wataungana nao 2 na kujiunga na nyumba ya Yakobo. 1
Jeremiah 3:18Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaungana na nyumba ya Israeli, wao kwa pamoja watakuja kutoka nchi ya kaskazini hadi nchi niliyowapa baba zenu kama urithi.
Jeremiah 29:14Nitaonekana kwenu,” asema Bwana, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni,” asema Bwana.