1 Chronicles 21:8
Kisha Daudi akamwambia Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Sasa, ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
7Amri hii ilikuwa mbaya machoni pa Mungu pia; hivyo akaiadhibu Israeli.
9Bwana akamwambia Gadi, mwonaji wa Daudi,
Cross References
1 Samuel 13:13Samweli akasema, “Umetenda kwa upumbavu. Hukuyashika maagizo ya Bwana Mungu wako aliyokupa. Kama ungelitii, angeudumisha ufalme wako juu ya Israeli kwa wakati wote.
2 Samuel 12:13Ndipo Daudi akamjibu Nathani, “Nimefanya dhambi dhidi ya Bwana.” Nathani akamjibu, “ Bwana amekuondolea dhambi yako. Hutakufa.
2 Samuel 24:10Dhamiri ya Daudi ilishtuka baada ya kuwahesabu wapiganaji, naye akamwambia Bwana, “Nimefanya dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Ee Bwana, sasa ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”
Psalms 25:11Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, 2 unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi. 1
Psalms 51:1Ee Mungu, unihurumie, 2 kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, 1 kwa kadiri ya huruma yako kuu, 2 uyafute makosa yangu. 1
Hosea 14:2Chukueni maneno pamoja nanyi, 2 mkamrudie Bwana. 1 Mwambieni: 2 “Samehe dhambi zetu zote 1 na utupokee kwa neema, 2 ili tuweze kutoa matunda yetu 2 kama sadaka za mafahali. 1