1 Kings 7:21
Hiramu akasimamisha nguzo kwenye baraza ya Hekalu. Nguzo ya upande wa kusini akaiita Yakini, + 7:21 Yakini maana yake Mungu atafanya imara. na ile ya upande wa kaskazini Boazi. + 7:21 Boazi maana yake Ndani ya Mungu kuna nguvu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
22Mataji yaliyokuwa juu yalikuwa na umbo la yungiyungi. Hivyo kazi ya nguzo ikakamilika.
Cross References
Ruth 2:19Basi mkwewe akamuuliza, “Je, umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Abarikiwe mtu yule aliyekujali.” Ndipo Ruthu akamwambia mama mkwe wake juu ya yule ambaye yeye alikuwa amefanyia kazi katika shamba lake. Akasema, “Yule mtu niliyefanyia kazi kwake leo, anaitwa Boazi.”
2 Samuel 7:12Siku zako zitakapokwisha nawe ulale pamoja na baba zako, nitainua mzao wako aingie mahali pako, ambaye atatoka viunoni mwako, nami nitauimarisha ufalme wake.
1 Kings 7:12Ule ua mkuu ulizungukwa na ukuta wa safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa, kama ulivyokuwa ua wa ndani wa Hekalu la Bwana na baraza yake. 1 Samani Za Hekalu (2 Nyakati 4)
2 Chronicles 4:13yale makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo); 1
Isaiah 45:24Watasema kuhusu mimi, 2 ‘Katika Bwana peke yake 2 ndiko kuna haki na nguvu.’ ” 1 Wote ambao wamemkasirikia Mungu 2 watamjia yeye, nao watatahayarika. 1
Ezekiel 40:49Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbili + 40:49 Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4. kuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo.