1 Samweli 6:2
Wafilisti waliwaita makuhani wa Dagoni na waaguzi, na kuwaambia, “Tutafanya nini na hili Sanduku la Bwana? Tuambieni jinsi tutakavyolirudisha mahali pake.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
1Sanduku la Bwana lilipokuwa limekaa katika nchi ya Wafilisti kwa miezi saba,
Cross References
Genesis 41:8Asubuhi yake, alifadhaika akilini, hivyo akawaita waaguzi wote pamoja na watu wenye busara wa Misri. Walipokuja, Farao akawaeleza ndoto zake, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kumfasiria.
1 Samuel 5:8Basi wakawaita watawala wote wa Wafilisti pamoja na kuwauliza, “Tutafanya nini na hili Sanduku la Mungu wa Israeli?” Wakajibu, “Sanduku la Mungu wa Israeli na liende Gathi.” Basi wakalihamisha Sanduku la Mungu wa Israeli.
Isaiah 47:12“Endelea basi na uaguzi wako, 2 na wingi wa uchawi wako, 2 ambao umeutumikia tangu utoto wako. 1 Labda utafanikiwa, 2 labda unaweza ukasababisha hofu kuu. 1
Daniel 5:7Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waganga waletwe, naye akawaambia hawa wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya na kuniambia maana yake atavikwa nguo za zambarau, na kuvikwa mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atafanywa mtawala wa cheo cha tatu katika ufalme.”
Matthew 2:4Herode akawaita pamoja viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, akawauliza ni mahali gani ambapo Kristo + 2:4 Kristo maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta. angezaliwa.