1 Timothy 6:13
Nakuagiza mbele za Mungu avipaye vitu vyote uhai, na mbele za Kristo Yesu ambaye alipokuwa anashuhudia mbele ya Pontio Pilato alikiri ukiri mzuri,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
14uishike amri hii bila dosari wala lawama mpaka kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo,
Cross References
1 Samuel 2:6“ Bwana huua na huleta uhai, 2 hushusha chini mpaka kaburini + 2:6 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. na hufufua. 1
John 5:21Hakika kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale anaopenda.
John 14:6Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.
John 18:36Yesu akajibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, wafuasi wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini kama ilivyo, ufalme wangu hautoki hapa ulimwenguni.”
Acts 17:25Wala hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji chochote, kwa sababu yeye mwenyewe ndiye awapaye watu wote uhai na pumzi na vitu vyote.
1 Timothy 5:21Ninakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu na mbele za malaika wateule, shika maagizo haya pasipo ubaguzi wala upendeleo.