2 Chronicles 29:6
Baba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa Bwana Mungu wetu na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya Bwana wakamgeuzia visogo vyao.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Chronicles 28:2Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, na pia akasubu sanamu kwa ajili ya kuabudu Mabaali.
2 Chronicles 34:21“Nendeni mkamuulize Bwana kwa ajili yangu na kwa ajili ya mabaki walioko Israeli na Yuda kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya Bwana ni kubwa mno ambayo imemwagwa juu yetu kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la Bwana wala hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa katika Kitabu hiki.”
Ezra 9:7Tokea siku za babu zetu mpaka sasa, hatia yetu imekuwa kubwa. Kwa sababu ya dhambi zetu, sisi na wafalme wetu na makuhani wetu tumekabiliwa na vita, utumwa, kutekwa na kudhiliwa katika mikono ya wafalme wa kigeni, kama ilivyo leo.
Nehemiah 9:32“Basi sasa, Ee Mungu wetu, uliye mkuu, mwenye nguvu na Mungu wa kuogofya, mwenye kushika agano lake la upendo, usiache taabu hizi zote zionekane kuwa kitu kidogo mbele za macho yako, taabu hizi zilizotupata, juu ya wafalme wetu na viongozi, juu ya makuhani wetu na manabii, juu ya baba zetu na watu wako wote, tangu siku za wafalme wa Ashuru hadi leo.
Jeremiah 2:13“Watu wangu wametenda dhambi mbili: 2 Wameniacha mimi, 2 niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, 1 nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, 2 visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji. 1
Jeremiah 2:27Wanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’ 2 nalo jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’ 1 Wamenipa visogo vyao 2 wala hawakunigeuzia nyuso zao; 1 lakini wakiwa katika taabu, wanasema, 2 ‘Njoo utuokoe!’ 1