2 Chronicles 34:19
Mfalme aliposikia yale maneno ya Sheria, akayararua mavazi yake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And it came to pass, when the king had heard the words of the law, that he rent his clothes.
In Context
Cross References
Joshua 7:6Ndipo Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana, na akabakia hapo mpaka jioni. Wazee wa Israeli nao wakafanya vivyo hivyo wakatia mavumbi vichwani mwao.
2 Kings 22:11Mfalme aliposikia maneno ya kile Kitabu cha Sheria, akararua mavazi yake.
Nehemiah 8:9Ndipo Nehemia aliyekuwa mtawala, + 8:9 Au Tirshatha : jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi. Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliokuwa wakiwafundisha watu wakawaambia wote, “Siku hii ni takatifu kwa Bwana Mungu wenu. Msiomboleze wala msilie.” Kwa kuwa watu wote walikuwa wakilia walipokuwa wakisikiliza maneno ya ile Sheria.
Joel 2:13Rarueni mioyo yenu 2 na siyo mavazi yenu. 1 Mrudieni Bwana, Mungu wenu, 2 kwa maana yeye ndiye mwenye neema 2 na mwingi wa huruma, 1 si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, 2 huona huruma, hujizuia kuleta maafa. 1
Romans 7:7Tuseme nini basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, hasha! Lakini, isingekuwa kwa sababu ya sheria, nisingalijua dhambi. Nisingalijua kutamani ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.”
Galatians 3:10Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Alaaniwe kila mtu asiyeshikilia kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Sheria.”