Joel 2:13
Rarueni mioyo yenu 2 na siyo mavazi yenu. 1 Mrudieni Bwana, Mungu wenu, 2 kwa maana yeye ndiye mwenye neema 2 na mwingi wa huruma, 1 si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, 2 huona huruma, hujizuia kuleta maafa. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 37:29Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yosefu hayupo, alirarua nguo zake.
Exodus 34:6Bwana akapita mbele ya Mose, akitangaza, “ Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu,
2 Samuel 1:11Ndipo Daudi pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye wakazishika nguo zao na kuzirarua.
2 Kings 5:7Mara mfalme wa Israeli alipomaliza kuisoma ile barua, akararua mavazi yake na kusema, “Je, mimi ni Mungu? Je, mimi naweza kuua na kufufua tena? Kwa nini huyu mtu anamtuma mtu ili mimi nipate kumponya ukoma wake? Tazama jinsi anavyotafuta kuanzisha ugomvi nami!”
2 Kings 22:11Mfalme aliposikia maneno ya kile Kitabu cha Sheria, akararua mavazi yake.
2 Chronicles 6:27basi usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi.