2 Chronicles 5:13
Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru Bwana, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu Bwana wakisema: 1 “Yeye ni mwema; 2 upendo wake unadumu milele.” Ndipo Hekalu la Bwana likajazwa na wingu,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 40:34Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa Bwana ukaijaza Maskani ya Mungu.
1 Chronicles 16:4Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli:
2 Chronicles 7:1Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa Bwana ukalijaza Hekalu.
2 Chronicles 7:3Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa Bwana ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru Bwana wakisema, 1 “Yeye ni mwema; 2 upendo wake unadumu milele.”
2 Chronicles 20:21Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia Bwana na kumsifu katika utukufu wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema: 1 “Mshukuruni Bwana 2 kwa kuwa upendo wake wadumu milele.”
Ezra 3:11Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa Bwana hivi: 1 “Yeye ni mwema; 2 upendo wake kwa Israeli 2 wadumu milele.” Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa Bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya Bwana ulikuwa umewekwa.