2 Chronicles 6:18
“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani na wanadamu? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 29:46Nao watajua kuwa Mimi Ndimi Bwana Mungu wao, aliyewatoa Misri ili nipate kufanya makao miongoni mwao. Mimi Ndimi Bwana Mungu wao.
2 Chronicles 2:5“Hekalu nitakalolijenga litakuwa kubwa, kwa sababu Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote.
2 Chronicles 32:15Sasa basi, msikubali Hezekia awadanganye na kuwapotosha namna hii. Msimwamini, kwa kuwa hakuna mungu wa taifa lolote wala wa ufalme wowote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka mkononi mwangu au mkononi mwa baba zangu. Sembuse huyo mungu wenu atawaokoaje kutoka mkononi mwangu!”
Job 9:14“Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye? 2 Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye? 1
Psalms 68:18Ulipopanda juu, uliteka mateka, 2 ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu, 1 hata kutoka kwa wale walioasi, 2 ili wewe, Ee Bwana Mungu, upate kuishi huko. 1
Psalms 139:7Niende wapi nijiepushe na Roho yako? 2 Niende wapi niukimbie uso wako? 1