Exodus 29:46
Nao watajua kuwa Mimi Ndimi Bwana Mungu wao, aliyewatoa Misri ili nipate kufanya makao miongoni mwao. Mimi Ndimi Bwana Mungu wao.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
45Ndipo nitakapofanya makao miongoni mwa Waisraeli na kuwa Mungu wao.
Cross References
Exodus 20:2“Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. 1
Leviticus 11:44Mimi ndimi Bwana Mungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi wenyewe kwa kiumbe chochote kile kiendacho juu ya ardhi.
Leviticus 19:2“Sema na kusanyiko lote la Israeli na uwaambie: ‘Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi, Bwana Mungu wenu, ni mtakatifu.
Numbers 16:3Wakaja kama kikundi kuwapinga Mose na Aroni, wakawaambia, “Ninyi mmejitukuza sana! Kusanyiko hili lote ni takatifu, kila mmoja wao, naye Bwana yu pamoja nao. Kwa nini basi mmejitukuza wenyewe juu ya kusanyiko la Bwana?”
2 Chronicles 6:18“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani na wanadamu? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
Jeremiah 31:33“Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli 2 baada ya siku zile,” asema Bwana. 1 “Nitaweka sheria yangu katika nia zao, 2 na kuiandika mioyoni mwao. 1 Nitakuwa Mungu wao, 2 nao watakuwa watu wangu. 1