2 Chronicles 6:37
na kama watabadilika mioyo yao katika nchi wanakoshikiliwa mateka, nao wakatubu na kukulilia katika nchi ya utumwa na kusema, ‘Tumetenda dhambi, tumefanya makosa na tumetenda uovu’;
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 4:29Lakini kama mtamtafuta Bwana Mungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote.
2 Chronicles 7:14kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.
Nehemiah 1:6tega masikio yako, na ufungue macho yako, ili usikie maombi ya mtumishi wako anayoomba mbele yako usiku na mchana kwa ajili ya watumishi wako, watu wa Israeli. Ninaungama dhambi zetu sisi Waisraeli, pamoja na zangu na za nyumba ya baba yangu, tulizotenda dhidi yako.
Job 33:27Ndipo huja mbele za watu na kusema, 2 ‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki, 2 lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili. 1
Isaiah 64:6Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi, 2 nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu; 1 sisi sote tunasinyaa kama jani, 2 na kama upepo maovu yetu hutupeperusha. 1
Jeremiah 31:18“Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu: 2 ‘Ulinirudi kama ndama mkaidi, 2 nami nimekubali kutii. 1 Unirudishe, nami nitarudi, 2 kwa sababu wewe ndiwe Bwana, Mungu wangu. 1