2 Peter 2:6
kama aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kwa kuiteketeza kwa moto ikawa majivu, na kuifanya kuwa kielelezo kwa yale yatakayowapata wale wasiomcha Mungu;
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
7na kama alimwokoa Loti, mtu mwenye haki, ambaye alihuzunishwa na maisha machafu ya watu wapotovu
Cross References
Genesis 19:28Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka kwenye nchi, kama moshi utokao kwenye tanuru.
Deuteronomy 29:23Nchi yote itakuwa jaa linaloungua la chumvi na kiberiti: hakutakuwa kilichopandwa, hakutakuwa kinachochipua, wala hakutakuwa mimea inayoota juu yake. Itakuwa kama maangamizo ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, ambazo Bwana aliangamiza kwa hasira kali.
Jeremiah 50:40Kama vile Mungu alivyoangamiza Sodoma na Gomora 2 pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,” 4 asema Bwana, 1 “vivyo hivyo hakuna mtu yeyote 2 atakayeishi humo. 1 Naam, hakuna mtu yeyote 2 atakayekaa humo. 1
Hosea 11:8“Efraimu, ninawezaje kukuacha? 2 Ee Israeli, ninawezaje kukutoa? 1 Nitawezaje kukutendea kama Adma? 2 Nitawezaje kukufanya kama Seboimu? 1 Moyo wangu umegeuka ndani yangu, 2 huruma zangu zote zimeamshwa. 1
Zephaniah 2:9Hakika, kama niishivyo,” 2 asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 Mungu wa Israeli, 1 “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, 2 Waamoni kama Gomora: 1 mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, 2 nchi ya ukiwa milele. 1 Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; 2 mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.” 1
1 Corinthians 10:11Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia.