2 Samweli 19:43
Ndipo watu wa Israeli wakawajibu watu wa Yuda, “Tunayo haki mara kumi kwa mfalme; sisi tunahusika zaidi na Daudi kuliko ninyi. Kwa nini basi mnatudharau? Je, hatukuwa wa kwanza kuzungumza kuhusu kumrudisha mfalme nyumbani?” Lakini watu wa Yuda wakajibu kwa ukali hata zaidi kuliko watu wa Israeli.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Judges 9:23Mungu akaruhusu roho mbaya kati ya Abimeleki na watu wa Shekemu, nao watu wa Shekemu wakamtendea Abimeleki kwa hila.
2 Samuel 5:1Makabila yote ya Israeli yakamjia Daudi huko Hebroni na kumwambia, “Sisi tu nyama yako na damu yako hasa.
2 Samuel 19:14Aliipata mioyo ya watu wote wa Yuda kama vile walikuwa mtu mmoja. Wakapeleka ujumbe kwa mfalme, kusema, “Rudi, wewe na watu wako wote.”
2 Samuel 20:6Daudi akamwambia Abishai, “Sasa Sheba mwana wa Bikri atatuletea madhara zaidi kuliko alivyofanya Absalomu. Wachukue watu wa bwana wako na umfuatie, la sivyo atapata mji wenye ngome na kututoroka.”
1 Kings 12:16Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: 1 “Tuna fungu gani kwa Daudi? 2 Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese. 1 Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli! 2 Angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
Proverbs 15:1Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, 2 bali neno liumizalo huchochea hasira. 1