Proverbs 15:1
Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, 2 bali neno liumizalo huchochea hasira. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
A soft answer turneth away wrath: but grievous words stir up anger.
In Context
2Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, 2 bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu. 1
Cross References
Judges 8:3Mungu amewatia Orebu na Zeebu, hao viongozi wa Wamidiani, mikononi mwenu. Je, mimi niliweza kufanya nini kulinganisha na mlichofanya ninyi?” Aliposema hili, hasira yao dhidi yake ikatulia.
1 Samuel 25:10Nabali akawajibu watumishi wa Daudi, “Huyu Daudi ni nani? Huyu mwana wa Yese ni nani? Watumishi wengi wanakimbia kutoka kwa bwana zao siku hizi.
2 Samuel 19:43Ndipo watu wa Israeli wakawajibu watu wa Yuda, “Tunayo haki mara kumi kwa mfalme; sisi tunahusika zaidi na Daudi kuliko ninyi. Kwa nini basi mnatudharau? Je, hatukuwa wa kwanza kuzungumza kuhusu kumrudisha mfalme nyumbani?” Lakini watu wa Yuda wakajibu kwa ukali hata zaidi kuliko watu wa Israeli.
1 Kings 12:13Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Akikataa shauri alilopewa na wazee,
2 Chronicles 10:7Wakajibu, “Kama leo utakuwa mtumishi wa watu hawa na kuwahudumia na kuwapa jibu linaloridhisha, watakuwa watumishi wako daima.”
Proverbs 10:12Chuki huchochea faraka, 2 lakini upendo husitiri mabaya yote. 1