2 Timotheo 2:14
Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 12:21Msigeukie sanamu zisizofaa. Haziwezi kuwatendea jema, wala haziwezi kuwaokoa kwa sababu hazina maana.
Jeremiah 2:11Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? 2 (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) 1 Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao 2 kwa sanamu zisizofaa kitu. 1
Jeremiah 16:19Ee Bwana, nguvu zangu na ngome yangu, 2 kimbilio langu wakati wa taabu, 1 kwako mataifa yatakujia 2 kutoka miisho ya dunia na kusema, 1 “Baba zetu hawakuwa na chochote zaidi ya miungu ya uongo, 2 sanamu zisizofaa kitu 2 ambazo hazikuwafaidia lolote. 1
Jeremiah 23:36Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina mzigo wa Bwana,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe, na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai, Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wetu.
Matthew 16:26Kwa maana, je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Acts 15:24Tumesikia kwamba kuna baadhi ya watu waliokuja huko kutoka kwetu bila ruhusa yetu na kuwasumbua, wakiyataabisha mawazo yenu.